Mshauri wa Maafikiano Mchunguzi Maalum (CAO) hutekeleza kazi pamoja na jumuiya na mashirika yanayohusu raia duniani kote kuwasaidia kusuluhisha masuala yanayowahusu na yanayozunguka miradi ya IFC/MIGA. Sehemu hii inaelezea jinsi ya kusajili lalamiko kwa CAO na yale utakayotarajia kutoka kwa mambo yatakayofuata. Pitia pitia kesi zetu ili ujifunze mengi kuhusu kazi tunazofanya na jinsi tunavyo saidia kupata suluhisho.
Mshauri wa Maafikiano Mchunguzi Maalum (CAO) ni nini?
CAO ni utaratibu huru kwa miradi inayotegemezwa na uajenti wa sekta ya kibinafsi wa Kundi la Benki ya Dunia – Shirika la Fedha la Kimataifa (IFC) na Uajenti wa Dhamana wa Uwekezaji kati ya nchi Nyingi (MIGA). IFC na MIGA husimamia upunguzaji wa umaskini kupitia kwa ukuzaji wa sekta ya kibinafsi kwenye taifa duniani kote. Watu wanapoamini kuwa mradi wa IFC au MIGA unaweza kuwaletea madhara, wanaweza kuomba msaada kutoka kwa CAO ili kuhutubia masuala yanayowahusu. CAO hutekeleza kazi pamoja na wahusika wote muhimu wa mradi ili kupata suluhisho halisi ambazo huendeleza matokeo ya kijamii na ya kimazingira katika eneo.
Nani Anayeweza Kuleta Lalamiko?
Mtu ye yote binafsi, kundi, jamii au mhusika mwingine aweza kuleta lalamiko kwa CAO, ikiwa wanaamini wako, au wanaweza kuathiriwa na mradi au miradi ya IFC au MIGA. Malalamiko yaweza kuletwa na mwakilishi au shirika kwa niaba ya wale walioathiriwa.
Kigezo cha Kuleta Lalamiko ni Gani?
CAO wana vigezo tatu rahisi za ustahilifu ili lalamiko listahili kwa ukadiriaji:
- Lalamiko lihusishe mradi wa IFC au MIGA (pamoja na miradi inayofikiriwa)
- Lalamiko lihusike na masuala ya jamii na/au mazingira yanayoshirikisha mradi au miradi hiyo.
- Mlalamikaji awe ameamini kuwa wame, au wanaweza kuathiriwa na masuala ya jamii na/au mazingira yaliyoletwa.
Ni aina gani ya malalamiko yasiyo kubalika?
- CAO haikubali malalamiko ambayo hayatosherezi vigezo tatu vya ustahilifu. Kama malalamiko yanahusiana na mashirika mengine ya kifedha (Kama vile sio IFC au MIGA) CAO hujitahidi kuelekeza mlalamikaji kwa ofisi ifaayo.
- Malalamiko yaliyo na madai ya ulaghai na ufisadi huelekezwa katika ofisi ya uadilifu wa shirika la Benki ya Dunia. CAO pia hawawezi kuchambua malalamiko yanayohusiana na uamuzi wa kuwadia wa IFC na MIGA.
- CAO haikubali malalamiko yenye nia mbaya, ya upuuzi, au yaliyofanywa ili kupata faida ya mashindano.
Je, ninahitaji ushahidi wa kuunga mkono ili niweze kutoa dai langu?
La, hauhitaji kuwasilisha ushahidi wa kuunga mkono ili utoe lalamiko. Hata hivyo, ukitaka kuwasilisha vifaa vya ziada vya kuunga mkono kesi yako, umekaribishwa.
Je, ninaweza kuomba kuwe na usiri?
Ndiyo, CAO huchukulia usiri kwa uzito kabisa na, tukiombwa, hatutafichua utambulisho wa walalamikaji. Mahali kuna ombi la usiri, utaratibu wa kushughulikia lalamiko utakubalika kwa pamoja kati ya CAO na mlalamikaji. Zaidi ya hayo, vifaa vilivyowasilishwa na mlalamikaji kwa msingi wa uaminifu havitatolewa bila idhini yao.
Mara tu ninapowasilisha lalamiko, ni nini hufanyika?
CAO watathibitisha upokezi wa lalamiko lako kwa lugha ambayo liliwasilishwa. Kati ya siku 15 za kufanya kazi (bila kuhesabu wakati unaotakikana wa kutafsiri malalamiko na hati za kuambatanisha) CAO watakujulisha ikiwa lalamiko lako ni stahilifu kwa ukadiriaji zaidi. Kama linastahili, utapokea habari zaidi ukielezwa jinsi CAO watafanya kazi pamoja nawe ili kujadilia masuala yanayo kuhusu, na mtaalamu wa CAO atawasiliana nawe binafsi.
Utaratibu wa kushughulikia lalamiko hutekelezwa aje?
CAO hufuata utaratibu fulani kwa kila lalamiko na wamejitahidi kushughulikia malalamiko kwa wakati ufaao. Kama lalamiko limeridhisha vigezo tatu vya ustahilifu vya CAO:
- Kwanza Mchunguzi Maalum wa CAO hutekeleza kazi pamoja na mlalamikaji, mfadhili wa mradi, na washika madau wengine ili kuamua ikiwa wahusika wote pamoja waweza kuafikiana na kupata suluhisho linalokubalika kwa suala lililotokea.
- Kama wahusika hawako tayari au wameshindwa kukubaliana jinsi ya kusuluhisha suala hilo, CAO huafikiana kuandaa tathmini kulingana na kuafikiana kwa IFC/MIGA pamoja na kanuni husika na mwongozo wa jamii na mazingira ili kuamua ikiwa ukaguzi ni wa haki.
Tazama mwongozo wa utenda kazi wa CAO kwa maelezo zaidi na wakati ufaao.
Je, Mchunguzi Maalum wa CAO hushughulikiaje Lalamiko?
Mchunguzi Maalum wa CAO hufanya ukaguzi wa hali, na kusaidia wahusika kuamua njia mwafaka ya kusuluhisha lalamiko. Mchunguzi Maalum huwa hafanyi uamuzi kuhusu ustahilifu wa lalamiko, wala kulazimisha suluhisho au kupata lawama. Watalaamu hutekeleza kazi pamoja na wahusika kutambua njia badala na mikakati ya kujadili masuala. Yaweza kuhusisha uchunguzi wa ukweli wa pamoja, kurahisisha majadiliano kati ya washika madau, kuingilia kati ya mabishano ya wahusika au kuanzisha mazungumzo au mpango wa pamoja wa kufuatilia. Wachunguzi Maalum wa CAO huwa wamejifunza njia badala za kuamua ugomvi (ADR), ni wenye ustadi katika ukadiriaji wa ugomvi, upatanishi, na kurahisisha vyama vingi. Huwa tunatekeleza kazi pamoja na wapatanishi huru ambao wana uzoefu maalum wa nchi na ambao ni wataalamu wa kurahisisha na kuleta maridhiano kwenye miradi ya maendeleo. Pitia pitia kesi zetu uweze kuona mifano ya kazi zetu.
Wajibu wa Kuafikiana kwa CAO ni gani?
Ikiwa azimio la lalamiko haliwezekani pamoja na Mchunguzi wetu Maalum, kuafikiana kwa CAO huchukulia kesi hiyo. Sababu ya jambo hili “kuthibitisha kuafikiana” ni kukadiria ikiwa suala lililojitokeza kwenye lalamiko linaleta maswali kuhusu juhudi za IFC na MIGA za kijamii na za kimazingira zinazostahili kwenye mradi husika. CAO huongoza tathmini na, kama ukaguzi utahitajika, kikao huru kitakutanika ili kuchunguza masuala. Ugunduzi utatolewa kwa umma na CAO watasimamia utekelezaji wa mapendekezo mpaka wakati mradi utaafikiana. La muhimu, ukaguzi wa kuafikiana hulenga IFC na MIGA – sio mfadhili wa mradi (mteja wa sekta ya kibinafsi ambaye alipokea msaada kutoka kwa IFC/MIGA).
Ni kwa njia gani na ni wapi nitawasilisha lalamiko langu?
Ni lazima malalamiko yawasilishwe kwa maandishi na yanaweza kuwa katika lugha yo yote. Malalamiko yaweza kutumwa kwa njia ya imeli, faksi, posta au kupelekwa kwenye ofisi ya CAO huko Washington, DC. Kwa mwongozo wa jinsi ya kuandika lalamiko, tazama “Kigezo cha Barua ya Lalamiko” kilichopo hapo juu.
Wasiliana nasi
Ikiwa una swali kuhusu jinsi ya kuwasilisha lalamiko au kuhusu kazi ya CAO pamoja na maisha ya raia, tafadhali wasiliana nasi. Tunataka kusikia kutoka kwako.
Ofisi ya CAO
2121 Mtaa wa Pennsylvania, NW
Washington, DC 20433, USA
Simu: + 1 202 458 1973
Faksi: + 1 202 522 7400
Imeli: cao-compliance@ifc.org